The trap episode 2

 


Mzee Yakobo Kizito alitoa panga akamkata yule mamba, damu zilitapakaa katika ile bahari, baada ya kumaliza kumuua yule mamba alisogea mpaka kwenye ule mwili. Alishangaa zaidi alipouona ulikuwa mwili wa mwanamke, mmh!!, huyu alikuwa anafanya nini katika hii bahari alisema Mzee Yakobo Kizito, kisha akaubeba ule mwili wa mwanamke mpaka nchi kavu. Alipofika nchi kavu alianza kumchunguza yule mwanamke kama ni mzima au amekufa, alisogeza sikio lake kwenye kifua cha ule mwili, akagundua alikuwa akipumua.  Mmmh!!, mbona mapigo ya moyo yako chini, ngoja nimpeleke hospitali anaweza akapona, alisema Mzee Yakobo Kizito, huku akiwasha bajaji yake.


Dr. Tafadhali nisaidieni, huyu mgonjwa atakufa, wewe Mzee hebu punguza munkari kila sehemu Kuna taratibu zake inatakiwa ufuate utaratibu. Inatakiwa uende kwanza mapokezi. Huko mapokezi nikafanye nini wakati mgonjwa wangu ana hali mbaya?. Yalikuwa majibizano kati ya Dr. Gamba na Mzee Yakobo Kizito.


Ndipo mganga mkuu wa ile hospitali akasikia ule mzozo akaamua kusogea pale. "Jamani Kuna nini?, aliuliza mganga mkuu". Si huyu Dr. ananiambia eti hata mtibu mgonjwa wangu mpaka niende mapokezi. Mganga mkuu alimueleza kwa kina Mzee Yakobo Kizito jinsi taratibu zilivyo, lakini mgonjwa wake atapewa huduma kwa hiyo asiwe na hofu. Ghafla alipita Dr. Joseph Manoti, samahani  Dr. Manoti wewe ndo utasimamia matibabu ya huyu mgonjwa Sawa. Sawa Mganga Mkuu.


Baada ya saa tatu kupita Dr. Joseph Manoti, alitoka katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU). Mzee Yakobo nakuomba ofisini wangu. Mzee Yakobo aliingia katika ofisi ya Dr Joseph Manoti, mazungumzo yalianza kati ya Mzee Yakobo Kizito na Dr Joseph Manoti.


Niambie.... niambie, niambie Dr. mgonjwa wangu ameshapata fahamu au amekufa. "Mzee hebu tulia, mbona unaharaka sana, kabla ya yote nataka kujua huyu mwanamke ni nani yako?". Dr, hebu acha siasa naomba unambie kama yuko hai au laa?.


****

Tulipofika kwenye msitu huo, tukiwa bado tunashangaa tukasikia sauti ya mwanamke akipiga kelele, ikatulazimu tusogee ili tujue kuna tatizo gani?. Hamuwezi kuamini ila ukweli ni kwamba tulishuhudia wanaume wanne wakimbaka binti mwenye ulemavu wa ngozi(albino).


Jose alifanikiwa kuchukua video ya tukio zima, wakati Jose anaendelea kuchukua video, kumbe mmoja wa wale wanaume alituona na akawaambia wenzake: "Kimeumana, kimenunka." Mwanaume mmoja mwenye suti ya kijivu alihoji, Charles tatizo ni nini?.


"Boss hapa hapafai tena, nzi wameshanusa tizama kule",alisema Charles. Yule mwanaume mwenye suti ya kijivu alichukia sana akatoa amri tukamatwe. Tupige simu polisi tuwaambie sisi ni wasamaria wema kutoka msitu wa Magoroto. Haloo, simu iliita kisha ikapokelewa upande wa pili, ni sisi wasamaria wema kutoka msitu wa Magoroto tunaomba mfike haraka kuna vitendo vya ukatili vinafanyika hapa. Sawa tunakuja. Sawa polisi. Pumbavu sana hawa wanajifanya wasamaria wema wanaharibu mipango yetu, leo mtajuta washenzi ninyi,alisikika akisema yule mwanaume aliyevaa suti ya kijivu.  Tuliomba msamaha kwa wale wanaume wanne lakini haikusaidia kitu.


Wale wanaume walitupiga, kisha wakatuvua nguo, na kutuambia lazima mfanye kile mkuu atakachosema, Sawa. Sawa tuliitikia kwa kutikisa vichwa vyetu. Wakati Joel, anaendelea kusimulia, ghafla alifika askari magereza na kusema muda umeisha. Tafadhali afande tupe angalau dakika mbili tu, alisema mjomba, lakini polisi alishikilia msimamo wake:"Nimesema time is over, kwa nini hamuelewi".Alisonya afande huyo wa kike. Patron James, pamoja na mjomba wa wale mapacha waliamua kuondoka. Joel na Jose waliendelea kulia tu. Ghafla Mkuu wa magereza, Bw Nyanda Kadogosa aliwaita wale watoto mapacha kwa ajili ya mahojiano. 


Baada ya siku saba, mjomba wake Jose na Joel, alitafuta Mwanasheria ili akawatetee watoto hao na waliongozana mpaka katika Gereza la Upanga kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria, lakini mwanasheria huyo alivyojaribu kuwahoji hawakumpa ushirikiano na wala hawakuwa tayari kujibu maswali yake.


Ghafla Jose alimtazama mwanasheria pamoja na mjomba wake kwa jicho la chuki kisha akasema :Mhh! sijui mmekosa kazi?. Au mmetumwa nini?. Ondokeni hatuhitaji msaada wenu.


"Unasemaje mpwa wangu?. Mbona unajikatia tamaa?. Tafadhali usihuzunike kiasi hiki, bado nipo hai kumbukeni mama yenu aliacha maagizo kwamba nihakikishe mnaishi vizuri, alisema mjomba kisha akatoa mfuko wenye chakula nakuwapa wapwa zake, lakini cha ajabu hakuna aliyekubali kula kile chakula.  Mzee ninaona hapa Kuna tatizo kubwa hawa watoto wameshaathirika kisaikolojia Ilikuwa sauti ya Benard Muganyizi, mwanasheria aliyekodiwa kuwatetea Joel na Jose.


Lakini wakati mjomba wake Joel na Jose na mwanasheria wakiendelea kushangazwa na msimamo wa watoto hao waliokuwa nyuma ya nondo za gereza.Ilisikika sauti ya askari magereza akisema :"mbona ninyi ni ving'ang'anizi mmeambiwa muondoke, lakini mnajifanya jeuri." Mjomba wa wale mapacha na mwanasheria walitizamana usoni kwa sekunde kadhaa kisha wakawatazama wale mapacha. Ndipo walipoamua kuondoka pale huku askari magereza akiwasindikiza kwa macho na kuwaambia "mlijifanya ameweka pamba kwenye masikio. Maana wale mapacha waliwaambia mapema muondoke lakini mkajizima data. Mjomba wa wale mapacha alimkata jicho yule askari


Itaendelea.... 

Dr Manoti anataka kujua yule mwanamke aliyeokotwa baharini ni nani?. Mzee Yakobo Kizito analalamika kwamba Dr Manoti Aache siasa amwambie ukweli kama yule mwanamke amepona au laa!.  Lakini upande mwingine  Mapacha wanakataa kula chakula kilicholetwa na mjomba wao huku wakimkataa mwanasheria pamoja na mjomba wao wakiongea kwa hasira kwamba mjomba na mwanasheria waondoke pale mahabusu.  Je, nini kitafuatia usikose kusoma sehemu ya tatu ya hadithi yako nzuri ya THE TRAP.. 

Post a Comment

0 Comments